Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido anunua saa ya mkononi Bilioni 1.2

IMG 20220328 WA0055 Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke "Davido"

Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: dar24.com

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu Davido bado anaendelea kuzikama Headlines kote barani Afrika kutokana na kuendelea kuonyesha jeuri ya pesa anazomiliki kwa kununua vitu vyenye thamani ya juu.

Baada ya kuongeza idadi ya magari ya thamani nyumbani kwake sasa ni zamu ya nyota huyo kuendelea kuuvalisha mwili wake bidhaa zenye thamani isiyo ya kawaida kiasi cha kuendelea kuzua gumzo kote barani Afrika.

Leo Machi 28, 2022 mwanamuziki huyo ameripotiwa kununua saa ya mkononi aina ya Richard Mille ‘RM11-02 18K’ yenye thamani ya usd 550k ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 za Kitanzania.

Ukiachilia mbali magari na mali nyingine za thamani anazomiliki nyota huyo, hii sio mara ya kwanza kwa yeye kununua saa yenye thamani kubwa, mnamo mwaka 2018 Davido aliwahi kununua saa ya thamani yenye madini ya Almasi.

Chanzo: dar24.com