Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Damian Soul kujitoa tuzo za TMA

Damian Pic Data Damian Soul

Sun, 20 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Siku moja baada ya Baraza Sanaa la Taifa (Basata) kutaja majina ya wateule watakaowania tuzo za muziki Tanzania (TMA), na kumtaja msanii Damian Soul kuwania kipengele cha msanii chipukizi, mwenyewe ageuka mbogo.

Wakati Damian akisema hayo, jana wakati Basata inatangaza matokeo hayo walikumbana na maswali ya waandishi kwa nini wamemuweka kipengele hiko, walisema alijichagulia wakati wa kuwasilisha kazi yake.

Akizungumza leo Jumapili Machi, 2022, Damian ambaye jina lake halisi ni Damian Mihayo amesema hajaridhika na kipengele alichopangwa na alichoamua ni kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa kuwa kipengele alichowekwa sicho alichojipendekeza kama masharti waliyokuwa wamepewa ya msanii kujiweka anapoona anafaa.

Katika kipengele cha chipukizi, Damian anashindanishwa na wasanii Kusah, Lody Music, Rapcha na Knata MC anayeimba nyimbo za singeli.

Katika kulipinga hilo, Damian anabainisha kuwa "Kupitia kampuni ninayofanya nayo kazi zangu za muziki ya Slide Vision, nilijipendekeza kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka nikiamini kibao changu cha mapopo ndipo kilistahili hapo.

" Pamoja na hayo iweje leo nijikute katika kipengele cha wasanii chipukizi wakati mimi nimeanza muziki miaka 10 iliyopita na nilishawahi kutajwa hata kwenye tuzo za KMA mwaka 2013, hii pia inaonyesha wazi baraza halinijui na hata kamati ya kuchagua majina haijui historia za wasanii.

"Huku ni kunikosea kikubwa na kunidhalilisha mbele ya mashabiki zangu ambao wanajua uwezo wangu, naomba niseme sitaki kushiriki hizo tuzo zao," amesema Damian aliyetingisha na kibao hiko cha mapopo kilicho katika mahadhi ya amapiano na kutesa sana kwa mwaka 2021.

Ni kutokana na hilo, amesema pia yupo katika kuwasiliana na mwanasheria kuona nini wanafanya zaidi huku akitaka serikali kusimamia kwa karibu tuzo hizo kwa kuwa kuna wajanja wameingia humo wanataka kusukuma proganda zao na kuzitumia kisiasa.

Tuzo za TMA zinatarajiwa kutolewa Aprili 1, mwaka huu ikiwa imepita miaka sita kusitishwa kutolewa kwa tuzo za muziki nchini, huku kipengele 51 vikiwa vinawaniwa na wasanii wanaofanya muziki wa aina mbalimbali.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz