Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DJ Joozey: Nilikuwa nalala na dada, mama yangu chumba kimoja na kuku, kondoo

Joosey DJ Joozey

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joseph Simon maarufu kama DJ Joozey ni miongoni mwa ma-DJ maarufu duniani kutoka Tanzania ambaye amefanikiwa kufanya kazi na mastaa wakubwa nchini Marekani akiwemo DJ Khaled.

Leo DJ Joozey ni moja ya Madj maarufu na wanaopata deals kubwa ndani na nje ya nchi. Hata hivyo safari yake ya kuwa Dj itakushangaza hasa kwakuwa ametokea kwenye familia maskini na kijijini Munze huko Kishapu, mkoani Shinyanga.

“Kwetu tupo watoto wanne watoto wawili ambao wakubwa zangu wao walibaki kwa Baba yao ila mimi na dada yangu tuliishi na mama ambapo tulikuwa tukikaa chumba kimoja na kwenye hicho chumba kilikuwa kilabu cha pombe kwa sababu mama yangu alikuwa akiuza pombe za kienyeji.

“Mama alikuwa akiuza pombe ndani ya chumba alichopanga na unakuta usiku wateja wa pombe wamekuja wanakunywa na sisi tupo ndani wadogo hivyo kama unavyojua walevi wengine wanazima hapo hapo asubuhi ikifika unaamka unajiandaa na kwenda shule.

“Hatukuwa na hela ya kununua hata kitanda hivyo nikatengeneza kitanda cha mbao na ndiyo tukawa tunalala kwenye kitanda hicho kwani maisha yalikuwa magumu sana. Tulikuwa tunalala na kuku na kondoo wawili wa mama.

“Kutokana na ugumu wa maisha niliamua kuacha shule nikiwa darasa la tatu, nikaanza harakati za maisha. Sikuwa na pesa, mama yangu aliuza kongoo wake mmoja kwa Tsh 35,000 akanipa pesa ya kuja kuanzia maisha Dar es Salaam.

“Nilipata lifti ya gari moja lilikuwa likitoka Mwanza, nikafanikiwa mpaka kufika Dar nikafikia kwa mshikaji wangu Tandale, baadaye nikaajiriwa kazi ya umachinga Kariakoo, nikanunusa simu ndipo nikaanza kuupenda muziki kama faraja pekee kutokana na hali yangu ya ufukara.

“Baadaye kuna jamaa alikuja anauza kompyuta kwa Tsh 60,000 nikampa tsh 40,000 na bosi wangu akanikopesha Tsh 20,000, pale ndipo nikaanza kuwa natengeneza mixtape zangu geto. Baadaye akaja rafiki yangu anaitwa Seif ndiye alinipa mchongo na kunipa moyo kuwa nafaa kuwa Dj, na jina langu la kwanza aliniita DJ Jose Black Simba, sababu nilikuwa nampenda Diamond Platnumz ‘Simba’.

“Sikuishia hapo, nikaenda kujiufnza U-DJ darasani, lakini baadaye ada ilikata nikarudi mtaani, nikawa nawasumbua Madj DM, mwisho wa siku Amour akanipokea na kunifundisha kazi mpaka nikawa DJ wa May Zone Club pale Masaki, hapo ndipo ulikuwa mwanzo wangu wa kuwa Dj mkubwa na kuyapata haya mafanikio.

“Mshahara wangu wa kwanza nililipwa Tsh 200,000, nilitaka kukimbia kwa sababu sikuwahi kushika laki mbili kwa pamoja… baadaye nikaenda Element Club na mwisho wa siku nikakutana na watu maarufu kutoka mataifa mbalimbali kunipa connection niliyo nayo leo," amesema Dj Joozey.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live