Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chance The Rapper atua Ghana

IMG 20220110 WA0016 Chance The Rapper atua Ghana

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: dar24.com

Siku chache zilizopita rapa mahiri kutoka nchini Marekani Chancelor Johnathan Bennett, maarufu Chance the rapper, alitembelea nchini Ghana akiwa na rapa mwenzake Vic Mensa.

Hii imekuwa mara yake ya kwanza kwa Chance the rapper kutembelea Ghana, ambapo safari hii imekuwa ya kutimiza mengi ambayo msanii huyo hakuwahi kukutana nayo kwenye maisha yake.

Chance the rapper na wenzake siku ya jana Jumapili ya januari 9, 2022. walifanikiwa kuhudhuria katika kanisa moja huko Accra ambapo rapper huyo alifichua kuwa bibi yake mkubwa alikuwa miongoni mwa watu waliosaidia kuanzishwa kwa kanisa hilo.

“Huyu askofu Nkansah, alimfahamu bibi yangu mkubwa,” aliandika kwenye moja ya video iliyorekodiwa kanisani wakati kiongozi wa ibada akihutubia.

Katika chapisho jingine, Chance The Rapper alifichua kuwa kwa kusema kuwa babu yake mkubwa alikuwa Muafrika na nahodha chini ya mwanaharakati Marcus Garvey.

Katika kuendelea kuthibisha historia ya familia yake na nchi ya Ghana Chance rapper aliweka picha yenye kuonyesha shule na kuamdika maneno yalisimeka “Walijenga Shule hii huko james Town pia”

Licha ya kusema hayo bado haijafahamika kwa undani zaidi ni mzazi yupi kati ya wazazi wa msanii huyo mwenye asili ya nchini Ghana.

Chanzo: dar24.com