Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boomplay na Capasso zaingia makubaliano ya kimkakati

Boom Pix Boomplay na Capasso zaingia makubaliano ya kimkakati

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: Mwananchi

Jukwaa linaloongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki, Boomplay limeingia makubaliano ya ushirikiano na Chama kinachosimamia hakimiliki za watunzi na waimbaji wa muziki (CAPASSO) ikiwa ni mkakati wa Boomplay kuendelea kupanua huduma zake barani Afrika.

Mpango huo unaifanya CAPASSO kuwa na mamlaka ya kukusanya na kusimamia mirabaha ya uchapishaji kwa niaba ya wasanii na watunzi wa maudhui mbalimbali ya muziki kutoka nchi tano hadi ishirini katika bara la Afrika.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi wa Maudhui na Mikakati wa Boomplay, Phil Choi amesema kuwa, leseni hiyo ya makubaliano inaendeleza maono na dhamira ya Kampuni kuuwezesha muziki wa kiafrika kuwa na uwezo, thamani na hadhi kubwa.

Phil amesema: “Tangu kuanza kwa ushirikiano wetu mwaka 2015, CAPASSO imekuwa mmoja wa washirika wetu wa karibu katika kuhakikisha watunzi barani Afrika wanapata sehemu ya haki yao ya mirabaha kupitia kazi zao. Shauku yetu kubwa ni kuhakikisha tunawajibika katika kuchangia kwa ukuaji mkubwa wa tasnia ya muziki barani Afrika kupitia ushirikiano wa kimkakati kama huu.

"Ushirikiano huu utaendelea kusaidia uwepo wa mfumo wa kuaminika wa kiikolojia kwa wasanii na wachapishaji, na tunaweza kutarajia kutengeneza njia zaidi za mapato kwa wasanii kupitia mtandao wa washirika wetu."

Jotam Matariro ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CAPASSO, ameunga mkono hoja za Choi, na kusema kuwa, "Lengo kuu la CAPASSO ni kuhakikisha kwamba watunzi wa nyimbo wa Kiafrika na wachapishaji wao wanapata thamani ya haki ya kazi zao. Hivyo ni fursa muhimu kushirikiana na wadau kama Boomplay, ambao mara kwa mara huwekeza katika mnyororo kamili wa thamani wa tasnia ya muziki wa Kiafrika. Ni kupitia utaratibu huo ndipo sekta nzima inaweza kuendelea kukua.”

Boomplay, ambayo inajivunia zaidi ya watumiaji milioni 60 kwa mwezi ikiwa na katalogi kubwa ya muziki yenye nyimbo zaidi ya milioni 60, ina shirikiana na lebo zote kubwa za ndani na nje ya Afrika na wasambazaji wa kazi za muziki. kuu zote na lebo na wasambazaji bora wa Kiafrika na Kimataifa.

Jukwaa hili hivi karibuni lilitangaza kuingiza takwimu za wasanii wa Afrika katika chati maarufu Duniani za Billboard.

Aidha, mafanikio haya na mengine mengi yamechangia kuimarisha nafasi zao katika kilele cha soko la upakuaji na usikilizaji muziki la Afrika.

Chanzo: Mwananchi