Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine ampa "Suprise" mkewe

IMG 20211222 WA0034 Bobi wine na Mkewe

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: dar24.com

Mwanamuziki na mwanasiasa maarufu kutoka nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu Bobi Wine, amemuandalia mke wake Barbie Itungo hafla maalum ya kushtukiza baada ya kuhitimu Shahada ya Uzamili ya Haki za Binadamu katika Chuo Kikuu cha London.

Bobi amemuandalia mke wake hafla ya kipekee iliyowaacha mashabiki vinywa wazi wakati ambao ushuhuda wa tukio hilo ukiiibua gumzo kote mitandaoni huku mamia ya mashabiki wa familia hiyo wakionyesha kuvutiwa sana na mfumo aliotumia mwasiasa huyo kumpongeza mke wake.

Kwa mujibu wa mke wa Bobi Wine, Bi. Barbie, amesema kuwa Bobi Wine amekuwa na uratatibu wa kumfuata uwanja wa ndege mara zote anaporejea kutoka masomoni, na alifanya vivyo hivyo hata aliporudi nchini mnamo Desemba 13, 2021.

Hilo halikumpa Barbie mawazo yoyote kuhusu kile ambacho kilikuwa kinamngoja nyumbani.⁣ .”Nikiwa nimechelewa na nimechoka, tarehe 13 Desemba 2021, nilifika nyumbani kwa mshangao mkubwa.

Niliwakuta wazazi wangu, ndugu zangu, wakwe zangu, Shangazi wa baba/mama wajawazito, wajomba na marafiki zangu wa karibu wamekusanyika kusherehekea pamoja nami mafanikio yangu mapya ya kitaaluma ya Digrii ya Uzamili ya Haki za Binadamu.” alisema Barbie.

“Sikushuku kwamba alikuwa amepanga mojawapo ya mikusanyiko hiyo mizuri ya familia ili kusherehekea Kuhitimu kwangu.

Asante Taata, nakupenda na bila shaka, nitalipiza kisasi hivi karibuni,” Barbie aliongeza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook⁣ .

Ni tukio gani Jema ambalo ni la kushtukiza Ulilowahi kufanyiwa na mwenzi wako na hutokuja kusahau

Chanzo: dar24.com