Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Big Sean adhamiria kutoboa siri za Kanye na GOOD MUSIC

Big Sean Big Sean

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda mfupi tu, baada ya Kanye West kutamka kujutia uamuzi wake wa kumsaini Big Sean kwenye Label yake GOOD MUSIC, maneno aliyoyazungumza kupitia kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha runinga Drink Champs yaliyoruka Novemba 5, 2021, kupitia Revolttv.

Inaonyesha wazi kuwa rapa Big Sean ameumizwa sana na kauli ya ‘YE’ kiasi cha kuchukua hatua ya kufululiza kutuma jumbe kadhaa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akidai kuwa yuko tayari kufanya mahojiano na kituo kilicho muhoji Kanye, ili naye aweke mambo hadharani.

Big Sean kwa ili kuthibiti kuwa pengine ni kweli ameathirika na uwepo wake kwenye Lebal hiyo mpaka kuamua kujitoa, amerejea na tweet iliyoibua gumzo zaidi kuhusu sakata hilo, baada ya kuandika kuwa anamdai Kanye kiasi cha pesa kisichopungua Usd 6 Milioni ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 13 kwa pesa za Kitanzania.

Sakata hili limeibuka muda mfupi tu, tangu rapa Big Sean kutangaza rasmi kujiengua kutoka kwenye Label ya Kanye na kuamua kujitegemea kwa kufungua Label yake mwenyewe iitwayo ‘FF to Def Entertainment’

Kanye na Big Sean walianza kufanya kazi pamoja tangu mwaka 2007.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live