Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ben Pol, Frida Aman wabeba tuzo uhifadhi wa Mazingira

Tuzo.jpeg Ben Pol na Frida Aman baada ya kupokea tuzo zao

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasanii kunako game ya Bongo Flavour, Ben Pol na mwanadada wa kufoka foka Frida Aman wametunukiwa tuzo maalumu baada ya kuonesha mchango wao mkubwa katika Shughuli za Uhifadhi wa Mazingira.

Ben Pol na Frida wamepokea tuzo hizo kutoka Taasisi ya Lead Foundation kutokana na mchango wao katika shughuli za uhifadhi wa Mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.

Dkt. Jafo ameyasema hayo akifungua Kongamano la Kukomboa Ardhi iliyochakaa katika Nyanda kame za Tanzania sanjari na Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la Lead Foundation.

Amesema kuwa kongamano hilo linatoa taswira ya namna gani NGOs zinashiriki kikamilifu katika kusukuma mbele agenda ya mazingira nchini hivyo kuwajengea uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira.

Kongamano hili limeandaliwa na Lead Foundation na limeshirikisha wadau mbalimbali wa mazingira ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live