Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beka Flavour awachezesha viongozi "Cheza kwa Madoido" Bagamoyo Festival

Beka Pic Data Beka Flavour awachezesha viongozi "Cheza kwa Madoido" Bagamoyo Festival

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bagamoyo. Msanii wa muziki wa Bongofleva, Beka Flavour amewaamsha viongozi katika meza kuu na kuwachezesha wimbo wa Cheza kwa Madoido '.

Hilo limetokea  jana Alhamisi Oktoba 28, 2021 katika uzinduzi wa tamasha la Bagamoyo linalofanyika  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUba) kwa siku tatu.

Viongozi hao waliochezeshwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbasi , Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Abdallah, Ofisa Mtendaji wa TaSUba, Dk Herbert Makoye na Kasida Mgeni ambaye ni Katibu Tawala wa Bagamoyo.

Wimbo huo uliimbwa na Kundi la Yamoto lililokuwa likiundwa na wasanii wanne akiwemo Mbosso, Enock Bella,  Aslay, na Beka ambalo mwaka 2017 lilivunjika rasmi na kila mtu kuamua kufanya kazi kivyake.

Beka ambaye alipanda jukwaani saa tano usiku, pamoja na kuimba nyimbo zake zingine kama Siachani Nae, Poapoa, Kibenten alizozitoa akiwa msanii anayejitegemea, lakini alipoimba Cheza kwa Madoido viongozi hao uzalendo uliwashinda na kujikuta wanavamia jukwaa na kucheza naye.

Kilichovutia zaidi katika hilo ni pale Dk Abbasi alipocheza staili ya cheza kimadoido kwa kukunja mguu mmoja jambo lililofanya watu kumshangilia huku wengine wakipiga miluzi.

Mwingine aliyekuwa kivutio ni Ofisa Mtendaji wa Tasuba alipokuwa akicheza kwa kukatika mpaka chini.

Wakati kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Zainabu yeye alikuwa akicheza huku akimtunza fedha alizokuwa akizitoa kwenye pochi yake.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz