Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi Nenda ilivyomchimbia kaburi Mo Music

Mo Music Basi Nenda ilivyomchimbia kaburi Mo Music

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mo Music anaingia kwenye orodha ya wasanii waliowahi kutoa nyimbo kali kuliko wao na nyimbo hizo zikaondoka na majina yao.

Back in Days game ya Bongo Fleva ilikuwa na wasanii kama J.I aliyeachia Kidato Kimoja, Bablee aliyewahi achia Kizizi, Chelah Man aliyeachia Usiniache/Msela, H. Mbizzo aliyeachia Mchumba Wangu.

Usimsahau BuiBui aliyeachia Nimekusamehe na wengine kibao, ngoma zao zilienda zaidi mjini na kuwameza, na hata walipotoa ngoma nyingine wakaonekana ni wa kawaida.

Neno wimbo wa Taifa, lilianzia kwenye Basi Nenda ya Mo Music miaka 8 iliyopita, ambapo msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' alishindwa kujizuia na kuupa wimbo huo hadhi ya wimbo wa taifa.

Sikumbuki kama kuna wimbo mwingine mbali na Basi Nenda uliwahi pewa hadhi hiyo hapo kabla licha ya kuwa kuna smash hits kibao ziliwahi toka nyuma. Wimbo huo ulifanya Mo Music afanye matamasha yote ya Serengeti Fiesta kwa mwaka 2014, na yale ya Kili Music Tour.

Baada ya hapo Mo Music hakuwahi toa wimbo uliowahi fikia Level za Basi Nenda, na sio kuwa hakuwa akitoa nyimbo kali, bali tayari Basi Nenda ilienda mbali zaidi kwa mashabiki na kuona nyimbo nyingine za msanii huyo ni za kawaida.

Kwenye The Chart ya 100.5 Times Fm, Mo music alidai Basi Nenda ilitoka kama wimbo wa majaribio, akiwaamisha mashabiki ana kazi kubwa zaidi ya wimbo huo, ambacho hakujua ni kuwa alijitungia mtihani mgumu sana ambao hadi leo hajawahi ufaulu hata kwa robo ya jumla ya marks ya mtihani.

“Nilikuwa naimani kwamba message, melody pamoja na vitu nilivyotengeneza nilkuwa naimani hii ingekuwa kubwa, lakini sio kwa ukubwa huo uliotokea kwa sasa hivi.

"Lakini kitu kikubwa nachoweza kusema ni kwamba hii Basi Nenda ilikuwa nyimbo ya Majaribio. Kwamba hii nyimbo ilikuwa plan B, kwamba tunaijaribisha hii nyimbo halafu inayokuja ndio itakuwa nyimbo inayotoka,” alisema Mo Music.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live