Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Barnaba ameamua kuweka wazi kuhusu kile kilichokuwa kikihoijiwa mitandaoni kwamba amefanya kolabu na wasanii karibu wote wakubwa Bongo lakini amemwacha Harmonize.
Akizungumzia hilo ikiwa ni siku chache baada ya kuachia albamu yake ya Love Sounds Different, Barnaba amesema alitamani sana kufanya kolabu hiyo lakini kilichotokea kilikuwa nje ya uwezo wake.
"Nimekutana na maswali hayo mengi sio tu kwa #Harmonize, ujue mimi ni mmoja wa watu ambao ni wanyenyekevu sana na niseme mtu yoyote ambaye nilimcheki sisemi alinisumbua lakini hakushiriki kwa muda ambao nilimuhitaji.
“Sijachukia kwa sababu naheshimu muda wa mtu, ujue kuna tabia moja ya wasanii ukimcheki msanii mwenzio kwa ajili ya kolabo akakwambia tutacheki kesho na kesho hivyo hivyo ikafika muda na wewe una mipango ukamkosa, hutakiwi kuchukia watu wana mipango na wapo busy.
"#Harmonize nilitamani awepo na nadhani watu ambao niliwacheki kwa muda mrefu ni yeye lakini naheshimu kitu alichokuwa anafanya, kwanza yupo busy.
“Na mimi kiukweli muda wangu ulikuwa umekata kwenye muda niliokuwa nataka kumfuata yeye. Ikawa siwezi tena kumkurupusha, sio vizuri ni kumkosea nidhamu, na hata mtu yoyote ambaye hajashiriki sina shida kwa sababu mimi naheshimu mipango ya watu," amesema Barnaba.