Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba aahidi kuandika historia mwaka 2022

IMG 20220330 WA0009 Barnaba boy

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: dar24.com

Mwanamuziki mahiri wa bongo fleva Elias Barnabas maarufu Barnaba boy, ametoa taarifa rasmi kuwa yuko katika maandalizi ya album yake mpya anayotarajia kuiachia siku za usoni na kwamba mpaka sasa imefikia kwenye hatua nzuri.

Barnaba amedai kuwa anachokiandaa kwenye album hiyo kitakwenda kuandika historia ya kipekee kutokana na namna alivyoamua kuifanya ya tofauti kwa kuwa ndio album yake pekee aliyochanganya mawazo yake na ya watu wengine.

Wasanii wengi aliowashirikisha ni wapya kwenye kiwanda cha muziki wa bongo fleva katika kuikamilisha album hiyo ambayo bado hajaweka wazi tarehe rasmi atakayoiingiza sokoni.

“Album yangu itakuwa bora kwa mwaka 2022 kwa sababu tatu, kwanza ni muziki uliotimia, second nimetoa nafasi kwa new generation kunipa mchango wa mawazo.

Lakini pia ndio album yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushirikisha wenzangu wengi kutoka ndani na nje ya nchi pia, i can’t wait wallahi bado naendelea kurekodi na nafanya final when i’m ready nitarudi kuwapa muongozo.”

Barnaba ameyasema hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram (Insta story) huku akiacha sintofahamu kwa mashabiki, maswali yakiwa je, ni wasanii gani kutoka nje ya Tanzania watakaosikika katika album hiyo?, na kwenye orodha ya wasanii chipukizi wenye kufanya vizuri nchini, jicho la Barnaba litakuwa limemchagua nani?

Chanzo: dar24.com