Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale: Basata, Cosota ni wababe

Hqdefault (600 X 450) Hamisi Taletale

Mon, 6 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Sanaa Tanzani (Basata) na Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) wametupiwa lawama kwamba hawana msaada wowote kwa wasanii badala yake wamekuwa ni maadui.

 Lawama hizo zimetolewa leo Jumatatu Juni 6, 2022 bungeni na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Taletale wakati akichangia hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Sanaa na Michezo kwa mwaka 2022/23.

“Basata imekuwa ni polisi, hawatoi elimu kwa wasanii badala yake wanasubiri kuwafungia wasanii pale wanapokosea, kila wakati wanawaza kuwafungia na wamekaa kwa kutegeshea,” amesema Taletale.

Mbunge huyo amedai baadhi ya watumishi katika Wizara ya Michezo wana roho mbaya zaidi hawafikirii kuwapeleka wasanii mbele ila wamejigeuza kuwa polisi.

Kuhusu Cosota amesema wakipelekwa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru) itawafunga wote kutokana na mazingira ya harufu ya rushwa kwenye kitengo hicho.

Advertisement Amedai kuwa Cosota haiangalii uwezo wa mtu katika sanaa badala yake wanatoa fedha za gawio bila kwa watu kwa majina siyo kwa kuangalia uwezo na mchango wao waliouonyesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live