Wed, 5 Jan 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
MREMBO maarufu wa Kenya aliyekuwa mke wa staa wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwaye Anerlisa Muigai amewataka wakosoaji wake kukaa mbali na uhusiano wa watu.
Kwa mujibu wa Anerlisa, ni dhabihu kubwa kufanya mambo yaende kwenye uhusiano kwa hiyo watu wawili hao wanapofurahia uhusiano wao wanapaswa kuachwa.
“Unapopata watu wawili wakiwa wamefurahi pamoja, tafadhali waache... watu hawajui ni bidii ngapi inafanywa ili kufanya mambo yaende,” anasema Anerlisa.
Alipotua Bongo hivi karibuni, mrembo huyo alidai kwamba ndoa ni jambo la kupewa heshima na wala siyo la kuongelelea kila mara na kila mtu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live