Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali kiba amkataa Diamond mbele ya waandishi

IMG 20211210 WA0006 Alikiba, msanii wa muziki wa BongoFleva

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ali Kiba kwa sasa yuko nchini Kenya alikokwenda kwaajili ya kutumbuiza kwenye moja ya matamasha aliloalikwa kama msanii rasmi.

Baaada ya kufika alipata wasaa wa kufanya mahojiano na vyombo mbali mbali vya habari nchini humo na kueleza mengi yenye kumuhusu ukiwa ni pamoja na maandalizi ya show yake anayotarajia kuifanya nchini humo.

Moja ya maswali aliyoulizwa Ali Kiba ni pamoja na hili la kuhusu kufungua kampuni ya kubashiri Michezo ‘Sports Betting Company’ kama ilivyo kwa msanii Diamond platnumz ambaye siku chache zilizopita alitangaza rasmi kuanza kufanya aina hiyo ya biashara akiinadi kwa jina la ‘WasafiBet’.

Kiba baada ya kuulizwa kama ana mpango huo, alisema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Dini yake haimruhusu.

“Kwa Bahati mbaya Dini yangu hairuhusu, lakini sasa sijajua Dini ya Diamond.” Alitoa jibu hilo mbele ya Waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuingia nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live