Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kiba ajibu "diss" ya Nikki Mbishi

Ali Kiba Ali Kiba

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapema siku ya leo Rapa Nikki Mbishi aliandika maneno katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, akidai kuwa muziki anaofanya Ali Kiba sio wa kuumiza kichwa sana wala wenye mambo makubwa zaidi ya chorus kali vinavyobaki ni kuunga unga tu.

Sasa Ali Kiba amejibu dongo hilo la Ney wa mitego kwa kusema kuwa pengine uelewa wake huyo aliosikiliza ndio umeishia hapo.

"Ni sawa kama yeye ameona hivyo basi uelewa wake ndio umeishia hapo, of course mziki ni lazima tuunge unge lakinu je unsleta sense?"

"Nikki Mbishi ni kaka yangu na nisingependa kulumbana nae, maana si unawajua tena vijana hawa, lakini cha msingi ni unamuacha mtu na kile anachokiamini katika akili yake" amesisitiza Kiba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live