Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

watu 30 wafariki duni anchini Myanmar

4061c96857ad1c83c090a7dabb4e0db6 watu 30 wafariki duni anchini Myanmar

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watu 38 wameuawa jana huko nchini Myanmar katika kile ambacho Umoja wa Mataifa umeelezea kuwa “siku ya umwagikaji mkubwa wa damu” tangu mapinduzi yalipofanyika mwezi mmoja uliopita.

Waandamanaji wamekuwa wakishinikiza kukomeshwa kwa utawala wa kijeshi na kuachiliwa huru kwa viongozi wa nchi hiyo waliochaguliwa – akiwemo Aung San Suu Kyi ambaye aling’olewa madarakani na kuzuiliwa wakati wa mapinduzi.

Uingereza imetoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, huku Marekani ikisema kuwa inatafakari kuwachukua hatua zaidi dhidi ya viongozi wa jeshi la Myanmar

Ghasia za hivi punde zinajiri siku moja baada ya majirani wa Myanmar kuomba majeshi kujizuia kufanya maafa zaidi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz