Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi kuhusu madai ya rushwa yanayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesema anataka kiongozi huyo wa zamani kuhukumiwa kifungo gerezani kwa kushindwa kufika mahakamani kujibu madai ya ufisadi yanayomkabili.
Jaji Ray Zondo anamshutumu Zuma kuidharau mahakama baada ya kudharau wito wa kufika mbele ya tume ya uchunguzi anayoongoza.
Hata hivyo Jacob Zuma amedai kwamba Jaji Zondo si mtu mzuri kwani alionesha upendeleo katika uamuzi alioutoa dhidi yake.
Mahakama ya kikatiba mwezi uliopita, ilitoa uamuzi wake na kusema kuwa Zuma analazimika kufika mbele ya tume hiyo.
Zuma anashutumiwa kuwa wakati wake madarakani, aliruhusu familia tajiri ya Gupta kupora mali ya serikali na kushawishi sera na uteuzi wa mawaziri, madai ambayo Zuma anaendelea kukanusha.