Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuma atafuta matibabu nchini Urusi

Zuma Atafuta Matibabu Nchini Urusi Zuma atafuta matibabu nchini Urusi

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma yuko Urusi Moscow kwa "sababu za kiafya", taasisi yake imesema.

"Atarejea [Afrika Kusini] mara tu madaktari wake watakapomaliza matibabu", taarifa kutoka kwa taasisi ya Jacob G Zuma iliendelea.

Habari hizi zinawadia siku moja baada ya Zuma kushindwa katika kesi katika Mahakama ya Kikatiba ambapo alijaribu kubatilisha uamuzi kwamba ni lazima arejee gerezani.

Rais huyo wa zamani aliondoka kuelekea Urusi wiki iliyopita kwa ndege ya kibiashara.

Siku ya Alhamisi Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba alipewa msamaha wa matibabu kinyume cha sheria.

Zuma alikuwa amepewa msamaha na mkuu wa zamani wa huduma ya magereza, Arthur Fraser, ambaye anachukuliwa kuwa mshirika wa rais huyo wa zamani.

Aliachiliwa mnamo Septemba 2021 baada ya kutumikia chini ya wiki nane za kifungo cha miezi 15 jela.

Zuma alikuwa amepatikana na hatia ya kudharau, baada ya kukataa kushirikiana na uchunguzi dhidi ya ufisadi katika kipindi chake cha uongozi.

Idara ya magereza imesema inachunguza uamuzi wa mahakama ya kikatiba na itatoa maoni yake baada ya kupata ushauri wa kisheria.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance kimefurahishwa na uamuzi wa mahakama ukisema kwamba unathibitisha kuwa Zuma "anatakiwa kuwa gerezani".

Chanzo: Bbc