Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuma apima umaarufu wake wa kisiasa katika kitongoji cha Soweto

Zuma Apima Umaarufu Wake Wa Kisiasa Katika Kitongoji Cha Soweto Zuma apima umaarufu wake wa kisiasa katika kitongoji cha Soweto

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma alionyesha nguvu zake katika kitongoji cha kihistoria cha Soweto alipokuwa akifanya kampeni za kutafuta kura katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Mei 29.

Wapiganaji wa Kizulu waliandamana kuzunguka Uwanja wa Orlando wakiwa na mikuki na ngao zao, wanaume waliojificha waliimba na kucheza nyimbo za mapinduzi, huku baadhi ya waimbaji maarufu wa Afrika Kusini - akiwemo rapa Big Zulu - wakitoa burudani kwa umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa Jumamosi.

Kwa wafuasi wa Bw Zuma mapinduzi makubwa yalikuwa ni kuwepo kwa mwanamume anayejulikana kama mfalme wa disko, Papa Penny.

Baada ya kutangaza kujiuzulu kutoka chama tawala cha African National Congress (ANC) wiki iliyopita, sasa amejiunga na chama kipya cha rais wa zamani, uMkhonto weSizwe, ambacho kinatafsiriwa kama Spear of the Nation. "Unganisha Afrika.

Unganisha Afrika Kusini," alisema katika hotuba fupi kwa umati wa watu, na kuongeza: "Phansi [Chini na] ukabila."

Chanzo: Bbc