Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuma akana mashtaka 18 yanayomkabili

Xqj4byyy848z8en88yv3 660x400.jpeg Zuma akana mashtaka 18 yanayomkabili

Wed, 26 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Leo May 26, 2021 Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesimama kizimbani na kukana mashtaka 18 yanayomkabili.

Katika kesi ya msingi iliyosikilizwa mahakamani Jijini Pietermaritzburg, mwanasiasa huyo anakabiliwa na tuhuma za rushwa, ukwepaji kodi na utakatishaji fedha.

Akizungumza kwa upole, huku watu wanaomuunga mkono wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama, Zuma mwenye umri wa miaka 79 amesema kesi zake ni matokeo ya siasa chafu dhidi yake.

Akifafanua hilo, Zuma hakuwataja majina lakini alisema maadui zake wanatoka ndani na nje ya Chama tawala, African National Congress (ANC).

TAZAMA MSAFARA WA MWANA WA KIFALME ULIVYOINGIA IKULU AKIKUTANA NA RAIS SAMIA

Chanzo: millardayo.com