Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuma agoma kufukuzwa ANC

Tume Ya Uchaguzi Afrika Kusini Yakataa Ombi Kumuondoa Zuma Kama Kiongozi Zuma agoma kufukuzwa ANC

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha uMkhonto weSizwe cha nchini Afrika Kusini kimesema kuwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma, atashirikisha timu yake ya mawakili kumtetea kufuatia hatua ya chama tawala cha ANC ya kumfukuza chamani baada ya chombo kimoja cha habari nchini humo kuweka wazi waraka uliovuja.

Waraka huo umeeleza kuwa Kamati ya Taifa ya Nidhamu ya chama cha ANC imempata Zuma na hatia ya kuathiri uadilifu wa chama baada ya kushirikiana na chama cha upinzani cha MK.

Zuma amekatiwa hukumu hiyo baada ya kusikilizwa kesi ya kinidhamu wiki iliyopita. Msemaji wa chama cha upinzani cha MK, Nhalamulo Ndhlela amesema hawatakaa kimya na kutazama kile alichokitaja kuwa kutotendewa haki kiongozi wao.

Chama cha upinzani cha MK kimeongeza kuwa kimeshtushwa na kusikitishwa na kuvuja kwa matokeo yaliyotolewa na Kamati ya Taifa ya Nidhamu, ambayo yamependekeza kwamba Zuma afukuzwe kutoka katika chama tawala cha ANC.

Wakati huo huo chama hicho kimesisitiza kuwa hakikuwahi kuarifiwa rasmi kuhusu kufukuzwa chamani Jacob Zuma, rais wa zamani wa Afrika Kusini.

Zuma ana muda wa siku 21 za kukataa rufaa dhidi ya uamuzi huo wa ANC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live