Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zulia jekundu la rais lililoibiwa Malawi lapatikana

Zulia Jekundu La Rais Lililoibiwa Malawi Lapatikana Zulia jekundu la rais lililoibiwa Malawi lapatikana

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: bbc

Polisi nchini Malawi wamepata zulia la rais lililokuwa limeibiwa katika mji wa kusini mwa Mwanza, karibu na mpaka na Msumbiji.

Zulia hilo liliibwa pamoja na hema usiku wa kuamkia Jumatano wakati bidhaa hizo zikihamishwa hadi mjini, ambapo Rais Lazarus Chakwera anatarajiwa kufanya hafla ya umma siku ya Ijumaa.

Wanaume wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, msemaji wa polisi Peter Kalaya alisema katika taarifa yake.

Wawili hao wanashukiwa kuiba vitu hivyo kutoka kwa gari la Wizara ya Uchukuzi na Utumishi wa Umma kando ya barabara ya Zalewa-Mwanza.

Rais Chakwera anatarajiwa jijini Mwanza kwa ajili ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja muhimu, pamoja na kukagua nyumba mpya za polisi zilizojengwa mjini humo.

Tukio hilo linakuja siku chache baada ya watu wasiojulikana kuvamia ofisi ya Makamu wa Rais Saulos Chilima katika mji mkuu wa Lilongwe na kuiba baadhi ya vitu.

Chanzo: bbc