Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zogo baada ya soja kumkaripia bosi wake aliyeshuku anashiriki ufuska na mkewe

534acef99a2115e4.jpeg Zogo baada ya soja kumkaripia bosi wake aliyeshuku anashiriki ufuska na mkewe

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kisanga kilitokea kwenye lango la kampuni moja mjini Ruiru, Nairobi bawabu alipomfungia nje meneja akidai alikuwa akimnyemelea mkewe.

Duru zinaarifu kuwa jamaa alikasirika na akachukua hatua hiyo baada ya kupata habari kuwa bosi wake alikuwa akichepuka na mama watoto.

“Leo hapa huingii. Siwezi fanya kazi halafu unaniendea kinyume. Kama unajiamini wewe ni mwanamume hebu karibia hili lango” lofa alimkemea mdosi wake jinis ilivyonukuliwa na Taifa Leo.

Inasemekana shughuli katika kampuni zilisimama huku kila mmoja akimshangilia jamaa kwa ujasiri wake.

“Fungia yeye nje, huyu mtu ni moto wa kuotea mbali,” wafanyakazi wengine walisikika wakisema.

Inasemekana askari huyo alianza kueleza namna bosi wake alivyokuwa akiingia nyumbani kwake kisiri.

“Kila siku ifikiapo saa saba huwa unatoka na gari lako. Sisi hufikiri kwamba huwa unaenda kutafuta chamcha lakini hapana. Chamcha chako huwa ni mke wangu,” mume wa bawabu alisema kwa hasira huku vicheko vikisikika.

Jamaa alieleza kuwa wakati mwingine bosi hupakua asali ndani ya gari.

“Huna aibu hata kidogo. Unawezaje kutumia gari lako kama lojing’i,” aliwaka.

Inaarifiwa kuwa soja alikuwa na hasira kupindukia na kuapa hatamfungu;ia mdosi mlango ili aingie ofisini.

“Walahi leo utasimama hapo hadi jioni. Lango sifungui na kama unajionea unatosha unga karibia hapa,” alitisha soja.

Semasema zinaarifu kuwa kwa kuhofia kuaibishwa zaidi, mdosi aliamua kugeuza gari na kurudi kwake.

“Enda kabisa. Ile siku tutakutana ana kwa ana utalaani siku uliyozaliwa,” jamaa alifoka.

Haikujulikana mwenye kampuni alichukua hatua gani baada ya kufahamishwa kisanga hicho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke