Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbambwe yatangaza hali ya dharura ugonjwa wa kipindupindu

Kipindupindu Kimeenea Kwa Kasi Barani Afrika WHO Zimbambwe yatangaza hali ya dharura ugonjwa wa kipindupindu

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Zimbabwe imetangaza hali ya dharura kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika mji mkuu wa Harare.

Tayari watu kadhaa wameripotiwa kufariki kutokana na maradhi yao wakati zaidi ya watu wengine elfu saba wakithibitishwa kuambukizwa.

Mamlaka ya jiji inasema msambao wa maambukizi hao kwenye jiji hilo, unatoa kumbukumbu ya kilichotokea mwaka mwa 2008 ambapo maelfu ya watu walifariki baada ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Meya wa jiji hilo la Harare, Ian Makone, akizungumza na vyombo vya habari vya ndani amethibitisha kutangazwa jwa hali hiyo ya dharura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live