Ongezeko la uchafu katikati ya jiji la Harare nchini Zimbabwe umezidi kumnyima usingizi Rais Emmerson Mnangagwa na sasa ametangaza hali ya janga ili kunusuru mji huo mkuu wa Taifa lililo Kusini mwa Afrika. - Mnangagwa amechapisha notisi ya tangazo hilo la hali ya hatari katika gazeti la serikali likitaja mji mkuu Harare kuwa umejaa taka zilizorundikana katika kila maeneo yakihusisha yale ya biashara na makazi. Taarifa imesema kumekuwa pia na uchomaji wa wazi wa taka na utapaji hovyo wa taka ngumu katika maeneo ya mji. - “Mamlaka za mitaa katika jimbo hilo zinashindwa kudhibiti uchafu huo kutokana na kushindwa kuwekeza katika miundombinu ya usimamizi wa taka na vifaa vinavyohusika na rasilimali watu na kutokuwepo kwa ufanisi katika ukusanyaji na mifumo ya udhibiti wa mazingira. - "Kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo taka ndani ya jimbo la mji mkuu wa Harare, hali ya maafa ipo katika jimbo hili na ndio msingi wa tamko hili," imeandikwa katika sehemu ya gazeti la serikali. - Gazeti la serikali lilitoa jukumu kwa Wakala wa Usimamizi wa Mazingira nchini (EMA) kuratibu uondoaji wa taka kwa “kuweka ramani, kupima na kusafisha dampo haramu na kuelekeza mamlaka za mitaa ndani ya jimbo la mji mkuu wa Harare kuanzisha vituo vilivyobuniwa na vilivyoteuliwa vya kuhamisha taka. ”. - Ikiwa na makadirio ya wakazi zaidi ya milioni 2, mji mkuu wa Harare una maeneo ya kutupa na uchafu lakini kumekuwa na uchafu unaorundikana mitaani kwa sababu ya kuzorota kwa utoaji wa huduma na kutokusanywa kwa taka na halmashauri ya jiji.