Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yawa miongoni mwa wazalishaji wakuu wa almasi duniani

ALMASI Zimbabwe yawa miongoni mwa wazalishaji wakuu wa almasi duniani

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimbabwe inashika nafasi ya saba kwa uzalishaji wa almasi duniani ikiwa na pato la kila mwaka la zaidi ya karati milioni 4 zenye thamani ya dola milioni 420 za Kimarekani.

Hayo yameripotiwa na Shirika la Utangazaji la Zimbabwe jana Jumatatu wakati lilipokuwa likinukuu takwimu za hivi karibuni kabisa za uzalishaji wa almasi kutoka kwa taasisi ya KPCS.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, takwimu zinaonesha kuwa, katika upande wa pato la madini ya almasi Zimbabwe iko nyuma ya nchi Botswana, Russia, Angola, Canada, Afrika Kusini na Namibia.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inalenga kuzalisha karati milioni 7 za almasi mwaka huu, na shabaha yake hasa ni kufikia mapato ya dola bilioni moja za almasi kila mwaka. Nchi za Afrika zina utajiri mkubwa wa maliasili lakini hazinufaiki ipasavyo na utajiri huo

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, malengo ya serikali ya Zimbabwe katika upande wa sekta ya madini ni kufikia pato la dola bilioni 12 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2023.

Nchi za Afrika zina utajiri mkubwa wa maliasili licha ya kwamba wananchi wake wanaishi katika viwango vya chini kabisa vya umaskini.

Ukoloni wa miaka mingi wa madola ya Magharibi barani Afrika, vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyochochewa na nchi hizo hizo za kikoloni za Magharibi, uongozi mbaya, ufisadi na ubadhirifu, uchu wa madaraka na kadhalika ni mionogni mwa mambo ambayo yanatajwa na wachambuzi wa mambo kuwa sababu za kuendelea wananchi wa nchi za Afrika kuishi kwenye lindi la umaskini na madeni licha ya bara hilo kuwa na utajiri mkubwa ambao unakodolewa macho ya tamaa na madola yote ya nje ya bara hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live