Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yatangaza hali ya hatari huku ukame ukiikumba nchi hiyo

Umoja Wa Mataifa Waomba Ufadhili Wa Haraka Kukabiliana Na Ukame Ethiopia Zimbabwe yatangaza hali ya hatari huku ukame ukiikumba nchi hiyo

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza hali ya hatari huku ukame ukiendelea kuikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Zimbabwe inakuwa nchi ya tatu barani Afrika kutangaza ukame kuwa janga la kitaifa, baada ya Zambia na Malawi.

Mnangagwa amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Harare kwamba nchi hiyo ina upungufu wa nafaka wa tani 680,000, huku zaidi ya watu milioni 2.7 wakihitaji msaada wa chakula.

Katika hotuba yake Rais wa Zimbabwe amesema: “Ndugu Wazimbabwe; Hali iliyotangulia ya ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi inahitaji hatua na uingiliaji kati kama ilivyoainishwa katika sheria zetu. Kwa sababu hiyo, ninatangaza hali ya maafa nchi nzima, kutokana na ukame unaosababishwa na El Nino."

Mnangagwa amesema nchi hiyo kwa sasa inategemea nafaka kutoka mataifa mengine. Zimbabwe ilipanda karibu hekta milioni 2 za mahindi ambayo yameunguzwa na joto la El-Nino. Emmerson Mnangagwa

Wiki iliyopita, Malawi ilitangaza hali ya maafa kutokana na ukame uliozikumba wilaya 23 kati ya 28. Rais Lazarus Chakwera wa nchi hiyo inayopakana na Tanzania alisema nchi yake inahitaji zaidi ya dola milioni 200 za msaada wa kibinadamu, chini ya mwezi mmoja baada ya nchi jirani ya Zambia pia kuomba msaada.

Zambia pia imetangaza hali ya ukame baada ya mavuno ya nafaka kufeli.

Zaidi ya watu milioni 6 nchini Zambia, milioni 3 kati yao wakiwa watoto, wameathiriwa na ukame. Hiyo ni karibu nusu ya wakazi wa Malawi na 30% ya Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live