Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yapiga marufuku mikusanyiko, kuuza chakula

Kipindupindu Kimeenea Kwa Kasi Barani Afrika WHO Zimbabwe yapiga marufuku mikusanyiko, kuuza chakula

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuongezeka kwa wagonjwa wa kipindupindu kutoka wagonjwa 437 wiki iliyopita hadi 1,259 wiki hii kumeifanya Serikali ya Zimbambwe ichukue hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuzuia mikusanyiko ya watu, uuzaji wa vyakula na kusimamia maziko katika maeneo yaliyoathirika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, visa vya kipindupindu nchini humo vimeongezeka mara tatu kutoka 437 hadi 1,259 wiki hii, hali ambayo ni mbaya zaidi tangu mlipuko huo mwezi Februari mwaka huu.

Hali hiyo, imezua hofu nchini Zimbabwe, huku kukiwa na kumbukumbu ya vifo vya zaidi ya watu 4,000 kutokana na kipindupindu mwaka 2008.

Hadi sasa nchi hiyo imerekodi vifo 155 vinavyohusishwa na kipindupindu huku visa vikiwa 8,787, kwa mujibu wa Wizara ya Afya.

Wiki iliyopita mamlaka nchini humo ilitangaza hali ya hatari katika mji mkuu wa Harare, ambao una idadi kubwa zaidi ya maambukizi mapya.

Siku ya Ijumaa, wakazi katika Kitongoji cha Kuwadzana, Harare, ambapo watu saba walifariki, walilalamika kuhusu usambazaji duni wa maji safi, takataka zisizokusanywa na maji taka yanayotiririka mitaani.

Wakazi wengi wamechimba visima vifupi ili kukidhi mahitaji yao ya maji.

"Maji kutoka kwenye visima pia yamechafuliwa. Wanatuhimiza kuchemsha maji kabla ya kunywa na kufika hospitali ikiwa tunahisi dalili," amesema Bertha Rwizi ambaye ni mgonjwa

Mhonjwa huyo ametoa kauli hiyo wakati akipatiwa matibabu katika Kliniki ya Polyclinic ya Kuwadzana, ambapo mamlaka wameweka mahema matatu ya matibabu ya dharura ya kipindupindu.

Mhudumu wa Afya, Mercy Chiweshe amesema maji safi ni muhimu katika kutibu wagonjwa wa kipindupindu na kuzuia maambukizi zaidi.

"Tunaomba visima kwa sababu uhaba wa maji unatuathiri na kwa wakazi kudumisha usafi," amesema.

Mamlaka ya Manispaa ya Harare imekuwa ikisambaza vidonge vya kutibu maji kwa wakazi kama sehemu ya juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live