Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yaomba kujiunga BRICS

Brics  Zimbabwe.jpeg Zimbabwe yaomba kujiunga na Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema kuwa nchi yake imetuma maombi ya kujiunga na Benki Mpya ya Maendeleo ya kundi la BRICS (NDB),

Rais Mnangagwa amesema hayo katika mkutano wake na Rais Vladimir Putin wa Russia mjini St. Petersburg.

Gazeti la Herald la Zimbabwe limeripoti habari hiyo na kumnukuu Mnangagwa akiongeza kuwa, nchi yake imewasilisha ombi la kujiunga na Benki Mpya ya Maendeleo ya Kundi la BRICS (NDB) na inatarajia kuungwa mkono na Russia.

Marais wa Zimbabwa na Russia katika mazungumzo ya pamoja mjini St. Petersburg

Rais wa Zimbabwe ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa Afrika waliohudhuria Kongamano la Pili la Uchumi na Masuala ya Kibinadamu la Russia na Afrika lililomalizika jana Ijumaa. Kongamano hilo limefanyika kabla ya mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS ambao utafanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi ujao wa Agosti.

Benki ya NDB ni taasisi ya fedha ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 2015 na nchi za BRICS, ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Madhumuni makuu ya kuanzishwa benki hiyo ni kufadhili miundombinu na miradi ya maendeleo endelevu katika nchi za BRICS na mataifa mengine yanayoibukia kiuchumi na nchi zinazoendelea kiujumla.

Hivi karibuni, Anil Sooklal, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Afrika Kusini katika kundi la BRICS alisema kuwa: Nchi 22 zimeomba rasmi kuwa wanachama katika kundi hilo.

Mwanadiplomasia wa huyo wa ngazi ya juu wa Afrika Kusini pia alisema, nchi kama Iran na Saudi Arabia zimeomba rasmi kuwa wanachama katika kundi la BRICS. Hadi sasa nchi zote wanachama wa BRICS zimeunga mkono na kukaribisha Iran kuwa mwanachama ndani ya kundi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live