Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yalaani vikwazo vipya vya Marekani na kuviita 'haramu na vya kukandamiza'

Zimbabwe Yalaani Vikwazo Vipya Vya Marekani Na Kuviita 'haramu Na Vya Kukandamiza' Zimbabwe yalaani vikwazo vipya vya Marekani na kuviita 'haramu na vya kukandamiza'

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Zimbabwe imelaani vikwazo vipya ambavyo Marekani iliweka dhidi ya rais na maafisa wakuu wa nchi hiyo siku ya Jumatatu.

Marekani ilimshutumu Rais Emmerson Mnangagwa na wengine kwenye orodha yake ya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Msemaji wa Rais Mnangagwa siku ya Jumatano alisema shutuma hizo ni za "kuwaharibia jina" na "kashfa zisizo na maana" dhidi ya viongozi na watu wa Zimbabwe.

Vikwazo hivyo vipya vilibadilisha mpango mpana ulioanzishwa miongo miwili iliyopita.

Naibu katibu mkuu katika timu ya mawasiliano ya Rais Mnangagwa George Charamba aliitaka Marekani kuondoa mara moja "hatua zisizo halali za kukandamiza".

"Tunalaani kauli hizi ovu na kusema kuwa hazifai kabisa, ni za kukashifu, za uchochezi, na kuendeleza uhasama mbaya dhidi ya Zimbabwe unaofanywa na serikali ya Marekani," alisema katika taarifa yake.

"Tunataka utawala wa Biden utoe ushahidi wa kuunga mkono shutuma hizi zisizo na msingi, na iwapo itashindwa, bila kuchelewa zaidi, iviondoe bila masharti."

Bw Charamba pia alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na jumuiya ya kanda ya kusini mwa Afrika Sadc kuunga mkono wito wa Zimbabwe wa kuondolewa kwa vikwazo hivyo.

Zimbabwe pia imekuwa ikikosoa jinsi serikali ya Marekani ilivyoondoa mpango wa zamani wa vikwazo siku ya Jumatatu, ikisema kuwa Wazimbabwe hawawezi kutarajiwa kushukuru kwa hatua hiyo.

Chanzo: Bbc