Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yaishukuru Rwanda kupigania vikwazo viondolewe

821bc032d8bff24aabbd661e82f260b2.jpeg Zimbabwe yaishukuru Rwanda kupigania vikwazo viondolewe

Tue, 18 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BALOZI wa Zimbabwe nchini, Charity Manyeruke amemshukuru Rais Paul Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha RPF-Inkotanyi, kwa kuendelea kusisitiza vikwazo vya kimataifa vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo viondolewe.

Balozi huyo alisema hayo wakati alipomtembelea Katibu Mkuu wa RPF-Inkotanyi, Francois Ngarambe katika makao makuu ya chama hicho tawala huko Rusororo juzi.

Alimshukuru Rais Kagame kwa kuendelea kusemea vikwazo vya kimataifa vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe viondolewe.

Vikwazo dhidi ya Zimbabwe viliwekwa wakati nchi hiyo ikiwa chini ya utawala wa Rais Robert Mugabe na kusababisha mdororo wa uchumi katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika kwa karibu miongo miwili sasa.

Kuhusu uhusiano wa nchi mbili, Balozi Manyeruke alisema mambo mengi yamefanikiwa tangu nchi hizo mbili zilizopoanza kuimarisha uhusiano na kila nchi kuwa na balozi mkazi katika mji mkuu.

“Kufikia sasa tumesaini makubaliano sita ya pande mbili katika maeneo tofauti ya ushirikiano. inaahidi kujitahidi kadri ya uwezo wangu kuendeleza uhusiano huu,” alisema.

Kwa upande wake, Ngarambe alimshukuru Balozi huyo na kuongeza kuwa kuna mengi ya kufanywa kati ya serikali zao na vyama vya RPF-Inkotanyi na ZANU-PF, vyama tawala vya nchi zote kwa maendeleo ya ustawi wa watu wan chi

Manyeruke aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kagame Novemba 2019 na kuwa Balozi wa kwanza wa Zimbabwe nchini Rwanda akiwa na makazi jijini Kigali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz