Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yafungua Makanisa yawaliochanjwa

MAKANISA Zibambwe kufungua Makanisa yawaliyochanjwa

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimbabwe imeanza kufungua makanisa, ambapo ni waumini waliopata chanjo ya corona ndio watakaoruhusiwa kushiriki ibada.

Mwezi uliopita mwanzoni mwa wimbi la tatu la janga la Covid-19 nchi hiyo ilipiga marufuku mikusanyiko ya watu ambayo ilihusisha huduma za ibada makanisani, mamlaka zilisema hali ilikuwa mbaya zaidi tangu mlipuko wa ugonjwa huo uanze mwaka jana.

Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa pia imejaribu kuongeza matumizi ya chanjo za Covid-19 kwa kuondoa posho kwa wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa na kuwazuia kutumia usafiri wa bure kwenda kazini.

"Makanisa sasa yanaweza kuwaruhusu waumini waliopata chanjo kamili au wale ambao wamechukua dozi mbili za chanjo kwa kufuata kanuni za kupamabana na Covid-19,"

Amesema Msemaji wa serikali Nick Mangwana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri jana.

Mangwana pia alisema kuwa viongozi wa makanisa watakaogundulika kukiuka agizo hilo watakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Wiki moja iliyopita, Zimbabwe ilifungua mipaka yake miwili kati ya Botswana na Zambia karibu na eleo la mapumziko la Victoria Falls kwa watalii ambao wamepewa chanjo dhidi ya Covid-19.

Hadi kufikia jana Jumatano Agosti 11, 2021, Wazimbabwe milioni 1.9 walikuwa wameshapokea dozi zote mbili za chanjo za corona wakati zaidi ya watu milioni moja walikuwa wamepewa chanjo kamili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live