Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yaanzisha kampeni ya chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kipindupindu

Zimbabwe Yaanzisha Kampeni Ya Chanjo Ya Nyumba Hadi Nyumba Ya Kipindupindu Zimbabwe yaanzisha kampeni ya chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kipindupindu

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: bbc

Zimbambwe imeanzisha kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa kipindupindi wakilenga zaidi ya watu milioni mbili dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa kupitia maji.

Mlipuko wa sasa ambao ulianza mapema mwaka jana umehusishwa na zaidi ya vifo 400 huku zaidi ya watu 21,000 wakisemekana kuambukizwa. Takriban nusu ya idadi hiyo ilihusisha watoto.

Kampeni ya chanjo inafanywa nyumba hadi nyumba kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa na inalenga raia kuanzia umri wa mwaka mmoja na zaidi.

Maafisa wa Afya wanatoa kipaumbele kwa wilaya 26 zinazochukuliwa kuwa kitovu cha ugonjwa huo.

Mlipuko huo umesababisha zaidi ya maambukizi 188,000 na zaidi ya vifo 3,000, hasa Zimbabwe, Msumbiji na Zambia, Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu, Ocha, linasema.

Chanzo: bbc