Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe yaanza mchakato kuwalipa wakopeshaji wakubwa

Zimbabwe.png Zimbabwe yajipanga kulwalipa wakopeshaji wakubwa kimataifa

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya nchini Zimbabwe, imesema kuwa imejipanga rasmi kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kusafisha taswira ya nchi hiyo.

Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Fedha wa nchini humo, Mthuli Ncube, na kusema kuwa tayari wameshalipa awamu ya kwanza ya deni wanalodaiwa na kikundi cha nchi tajiri kinachojulikana kama 'Paris Club'.

"Tumesha anza kuwalipa,kwa sababu kama taifa ni vyema tukajulikana kama walipaji wazuri kuliko wakopaji wabaya" amsema Waziri huyo.

Ameongeza kusema kuwa, tayari wanafanya mchakato wa kuwalipa wakopeshaji wa kimataifa kama Benki Kuu ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya uwekezaji ya Marekani.

Nchi hiyo inadaiwa dola za kimarekani bilioni 11 sawa na trilioni 25.59 za Tanzania kutoka kwa wakopeshaji wa nje .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live