Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe katika jitihada za kuzuia kipindupindu

Kipindupindu Kimeenea Kwa Kasi Barani Afrika WHO Zimbabwe katika jitihada za kuzuia kipindupindu

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuchukua hatua za kudhibiti kuenea ugonjwa wa kipindupindu nchini humo ambapoo hadi sasa watu 5,000 wamepata maambukizi tangu mwezi Februari mwaka huu.

Zimbabwe inafanya kila iwezalo ili kuzuia kuenea kwa mlipuko wa kipindupindu, huku serikali ya nchi hiyo ikitangaza hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo. Hali ya wasiwasi imetanda juu ya uwezekano wa kukaririwa mlipuko kama ule wa mwaka 2008 huko Zimbabwe ambao ulipelekea kutangazwa dharura ya kitaifa.

Hadi sasa maambukizi kadhaa ya ugonjwa wa kipindupindu yameripotiwa katika majimbo yote 10 ya Zimbabwe, huku kukiwa na ongezeko la kutisha zaidi katika majimbo ya kusini-mashariki ya Masvingo na Manicaland. Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa kipindupindu kimeuwa watu zaidi ya 100 na kuambukiza wengine 5,000 nchini humo tangu mwezi Februari mwaka huu. Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu Zimbabwe

Tayari serikali ya Harare imetangaza hatua kadhaa za kuzuia kuenea maambukizi ikiwa ni pamoja na kuzuia safari katika maeneo yaliyoathirika, kupunguza idadi ya watu mazikoni hadi 50 na kuzuia watu kusalimiana kwa kupeana mikono au kugawa chakula katika maeneo ya mikutano, sherehe n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live