Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe imewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani

Zimbabwe Imewafungulia Mashtaka Wanaharakati 39 Wa Upinzani Zimbabwe imewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Voa

Waendesha mashtaka wamesema kundi hilo lilishambulia ofisi ya chama tawala cha ZANU-PF, katika eneo la Nyatsime, kusini mwa mji mkuu, wiki iliyopita. Chama tawala cha ZANU-PF kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980

Mamlaka nchini Zimbabwe zimewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani wanaoshutumiwa kuzua ghasia za kisiasa kuhusiana na madai ya kuharibu ofisi ya chama tawala siku ya Jumatatu wakati mvutano ukiongezeka kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Agosti.

Waendesha mashtaka wamesema kundi hilo lilishambulia ofisi ya chama tawala cha ZANU-PF, katika eneo la Nyatsime, kusini mwa mji mkuu, wiki iliyopita. Chama tawala cha ZANU-PF kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980.

Kundi hilo liliharibu nyumba kadhaa na pia kuwashambulia watu wa jamii ya Nyatsime na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kusababisha majeraha makubwa kwao, waendesha mashtaka walisema.

Tukio hilo limekuja wakati makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani nchini humo vikilalamikia kukandamizwa kuelekea uchaguzi mkuu. Mawakili wa watu waliokamatwa, hata hivyo, waliashiria kuwa mashtaka hayo yalichochewa kisiasa.

Chanzo: Voa