Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimbabwe, Iran kufanya makubaliano mageuzi ya uchumi

Mjnhnakiishyrytrdndcnfcmj Zimbabwe, Iran kufanya makubaliano mageuzi ya uchumi

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikao cha tisa cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Zimbabwe kimefanyika hapa mjini Tehran.

Kikao cha tisa cha Kamisheni ya Pamoja ya Kiuchumi ya Iran na Zimbabwe kilichoanza tarehe Mosi ya mwezi huu wa Februari hapa mjini Tehran jana kilishuhudia kutiwa saini hati ya ushirikiano baina ya Waziri wa Ushirika, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Iran na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari pambizoni mwa mkutano huo Sayyid Solat Mortazavi, Waziri wa Ushirika, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumefikiwa makubaliano baina ya pande bili ambayo yanatabiri ongezeko la ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa haya mawili ambalo litafikia kiwango cha zaidi ya dola milioni 500 kwa mwaka.

Aidha amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zimefikia katika hatua nzuri kwenye mazungumzo na kwamba, serikali ya Harare ina nia ya dhati ya kushirikiana zaidi na Tehran na kunufaika na uzoefu wa taifa hili katikak nyanja mbalimbali.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitoa kipaumbele katika sera zake za kigeni juu ya kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Kiafrika na kuitaja Afrika kwamba, ina nafasi maalumu katikak sera za kigeni za Tehran.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live