Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziara ya Rais Samia yaongeza biashara ya Mahindi Tanzania Kenya

Maize Rais wa Kenya,Uhuru kenyatta (Kulia) na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan(wa pili kushoto)

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya umeongezeka maradufu hadi kufikia magunia 118,329 Kufikia Mwezi Mei baada ya ziara ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Kenya .

Wizara ya Kilimo nchini Kenya imesema idadi hiyo iliongezeka kutoka magunia 16,137 Aprili hadi 118,329 Mei baada ya Rais Samia na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta kufikia makubaliano ya kumaliza vizuizi baina ya nchi hizo mbili ambavyo Serikali ya Kenya ilikuwa imeweka kwa mahindi yanayotokea chini Tanzania.

Mnamo Mwezi Aprili ,Kenya ilipiga marufuku uingiaji wa mahindi kutoka Tanzania na Uganda.

"Biashara isiyo rasmi ya mpakani iliripoti kuwa jumla ya uagizaji wa mahindi kwa mwezi Aprili ilikuwa magunia 16,731. Mnamo Mei, uagizaji uliongezeka hadi magunia 118,329, ā€¯ilisema wizara hiyo.

"Uingiaji wa mahindi ulipungua katika kipindi cha mwezi Aprili na hali hiyo ilisababishwa na katazo lililokuwa limewekwa awali kuzuia uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania".

Nchi ya Kenya kwa kiasi kikubwa inategemea kuagiza mahindi kutoka nchi za Tanzania na Uganda.

Ili kurahisisha masuala ya Kibiashara baina ya nchi hizo mbili, hivi karibuni Tanzania ilikubali kuondoa ada ya ukaguzi wa bidhaa zilizosindikwa zenye alama za usanifishaji kutoka Kenya.

Tanzania ilisema itaruhusu Juisi za Kenya na unga wa ngano kuingia soko la Tanzania kufuatia mkutano baina ya pande mbili ambao ulitatua vizuizi vya kibiashara ambavyo viliona bidhaa hizi zinakabiliwa na vikwazo vya kibali mpakani.

Aidha,nchi ya Tanzania ilisema imeanza kutekeleza Mfumo wa Dirisha Moja, ambao umepunguza ucheleweshaji wa vibali vya juisi ya mananasi inayozalishwa Kenya.

Mkutano huo ulielekeza Mamlaka ya Mapato ya Kenya na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kuchunguza uwezekano wa kutoa upendeleo kwa sigara inayotengenezwa nchini Kenya kwa tumbaku inayopatikana kutoka Tanzania na kuripoti katika mkutano ujao baina ya nchi hizo.

Ili kurahisisha mchakato wa usafirishaji wa bidhaa kati ya nchi hizi, iliafikiwa kuwa na Kituo cha Forodha kimoja, kitakachoshughulikia pande zote mbili kikamilifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live