Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ziara ya Mfalme Kenya yazua mwito mpya wa kurudishwa kwa fuvu

Ziara Ya Mfalme Kenya Yazua Mwito Mpya Wa Kurudishwa Kwa Fuvu Ziara ya Mfalme Kenya yazua mwito mpya wa kurudishwa kwa fuvu

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazee wa jamii ya Nandi nchini Kenya wametoa madai mapya kwa Uingereza kurudisha fuvu la Koitalel arap Samoei, chifu pamoja na kiongozi wa kiroho na kijeshi aliyeuawa na Waingereza mwaka 1905.

Matakwa hayo mapya yanakuja siku chache kabla ya ziara ya Mfalme Charles III nchini Kenya tarehe 31 Oktoba.

Samoei, ambaye aliongoza upinzani mkali dhidi ya wakoloni, aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza Kanali Richard Meinertzehagen, baada ya kuwalaghai Samoei na viongozi wengine wa Nandi kuhudhuria mkutano wa mapatano.

Kulingana na gazeti la Daily Nation la Kenya, wazee hao pia wanataka kurejeshewa vitu vyao vya kitamaduni vilivyoibiwa na kufidiwa kwa ukatili waliofanyiwa jamii wakati wa utawala wa kikoloni, ikiwa ni pamoja na mauaji, kuwekwa kizuizini na kuwahamisha watu wa jamii wa Nandi kwa nguvu.

Fuvu la Samoei linaaminika kuwa katika mkusanyiko wa makumbusho mahali fulani nchini Uingereza.

Wazee wa Nandi wameiomba mara kwa mara Uingereza kurejesha mabaki yake.

"Tunamsihi Mfalme Charles, tunahitaji kupata fuvu hilo ili lirudishwe Nandi kwa mazishi ya heshima," David Samoei aliambia kituo cha runinga cha KTN News mapema mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live