Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanu-PF haiingilii uchaguzi wetu, ANC yasisitiza

Zanu PF Haiingilii Uchaguzi Wetu, ANC Yasisitiza Zanu-PF haiingilii uchaguzi wetu, ANC yasisitiza

Fri, 10 May 2024 Chanzo: Bbc

Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC, kimetetea kualika chama tawala cha Zimbabwe nchini humo kabla ya uchaguzi.

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini kililaani mwaliko huo kama jaribio la "kuchafua" mchakato wa uchaguzi.

Chama cha Democratic Alliance (DA) kilisema ombi la Zanu-PF kuwa "sehemu ya programu ya kampeni ya uchaguzi [ya ANC] ni sawa na kuingiliwa kwa kisiasa na uchaguzi wetu".

DA ilisema Zanu-PF haikustahili kuwa mwangalizi katika uchaguzi huo, na kuongeza kuwa itawasilisha malalamishi yake kwa tume ya uchaguzi.

Kujibu suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa ANC Nomvula Mokonyane alishutumu upinzani kwa "mkanganyiko kati ya shughuli za chama na hadhi ya waangalizi kulingana na michakato ya [tume ya uchaguzi]".

Bi Mokonyane alisema ANC ilialika Zanu-PF nchini kama mgeni. Chama chake "kina utamaduni wa muda mrefu wa kualika vyama vya ukombozi kutoka katika bara zima la Afrika na kwingineko kama wageni", aliongeza.

Mapema wiki, gazeti linalodhibitiwa na serikali ya Zimbabwe lilimnukuu Katibu Mkuu wa Zanu-PF Obert Mpofu akisema chama hicho kimealikwa na ANC "kuwa sehemu ya mchakato wao wa uhamasishaji katika siku chache zilizopita za kampeni".

Chanzo: Bbc