Zambia imekanusha madai yaliotolewa na msemaji wa zamani wa waasi wa FNL mahakamani kwamba Rais Edgar Lungu alifadhili kundi hilo kushambulia Rwanda.
Mwaka jana , Callixte Nsabimana ambaye pia anajulikana kama Sankara, alikamatwa Comoros na kukabidhiwa kwa Rwanda, wakati huo alikuwa msemaji wa waasi wa FLN walio na makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliposhambulia maeneo ya kusini magharibi mwa Rwanda mwaka 2018.
Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya Jumatatu, Bw. Nsabimana alisema kupitia urafiki wake na kiongozi wa upinzani wa Rwanda, Rais Edgar Lungu aliwapatia waasi hao dola 150,000 kufanya mashambulio dhidi ya Rwanda
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zambia usiku wa Jumanne ilisema "Tunapinga vikali madai hayo" na kuongeza kuwa "madai hayo ni ya uwongo".
Bw.Nsabimana ambaye amekiri baadhi ya mashitaka 17 dhidi yake, pia amelaumu serikali za Burundi na Uganda kwa kuunga mkono waasi wa FLN, madai ambayo majirani hao wa kusini na kaskazini wa Rwanda waliwahi kukanusha.
Wapinzani wa Rwanda waliopo ughaibuni wanasema kile alichosema mahakamani Bw. Nsabimana ni "kile alichokubali kufanya baada ya mateso ya wiki nzima aliyopitia ili akubali kukiri makosa". Callixte Nsabimana Maelezo ya picha,
Meja Callixte Sankara aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi dhidi ya Rwanda la National Liberation Front Callixte Sankara ni nani?
Meja Callixte Sankara aliyekuwa msemaji wa kundi la National Liberation Front lililotangaza uasi dhidi ya Rwanda.
Kundi lake lilidai kuhusika na mashambulio dhidi ya vijiji vilivyo karibu na msitu wa Nyungwe kusini magharibi mwa Rwanda na kudai kuwa bado wapiganaji wake wana ngome katika msitu huo,madai yanayokanushwa na serikali ya Rwanda.
Kiongozi wa waasi Rwanda amekamatwa vipi? Meja Callixte Sankara ni nani?
Mnamo mwezi Mei 2019, Sankara alifikishwa mbele ya mahakama mjini Kigali ambapo amekiri mashtaka 16 dhidi yake na kuomba radhi.
Mwendesha mashtaka amesoma mashitaka 16 dhidi ya mshtakiwa ambayo yana uhusiano na ugaidi, ujambazi wa kutumia silaha na ushirikiano na nchi ya kigeni kwa lengo la kuishambulia Rwanda.
Kwa mjibu wa mwendesha mashtaka, nchi za Burundi na Uganda kuunga mkono harakati za kivita za kundi la National Liberation Front dhidi ya Rwanda akisema Burundi ilitoa njia na kuwapa ngome wapiganaji wa kundi hilo waliotumia msitu wa Kibira ambao unapakana na msitu wa Nyungwe waliopitia hadi kuishambulia Rwanda huku Uganda ikiwapa silaha na kusaidia wapiganaji waasi na kuwasaidia kwenda katika ngome zao zilizoko DRC. zambia
Na machache yanayojulikana kuhusu Callixte Sankara:
Mtu aliyejitangaza kama naibu kamanda na msemaji wa kundi jipya la waasi la Rwanda Movement for Democratic Change.
Meja Callixte Sankara, kama avyojitambulisha kwa vyombo vya habari, ni Mtutsi ambaye alinusurika maauji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.
Wazazi wake na jamaa wake wote waliuawa na wanamgambo wa Kihutu- Interahamwe.
Kwa sasa ana umri wa miaka 38.
Hakuwahi kuwa mwanajeshi wa RPF kwa kuwa RPF ilishika madaraka akiwa na umri wa kama miaka 10 tu.
Baada ya kuhitimu sheria katika chuo kikuu cha Rwanda- Butare, Callixte Sankara, alizozana na serikali ya Rwanda, akakimbilia Afrika ya kusini ambako alijiunga na NRC- Rwanda National Congress, ambayo ilibuniwa na Kayumba Nyamwasa, jenerali na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda.
Alikamatwa nchini Comoro mapema mwezi wa 4.