Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia yalegeza masharti ya Corona

Zambia Picdd Zambia yalegeza masharti ya Corona

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Zambia imetangaza kulegeza mashariti ya ugonjwa wa Corona nchini humo mara baada ya kupungua kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Taarifa hii imetolewa na Waziri wa Afya nchini humo Sylvia Masebo,na kusema kuwa tayari wameshatoa chanjo kwa zaidi ya asilimia tatu tangu zoezi hilo kuanza nchini humo.

"Kufuatia kupungua kwa kasi ya maambukizi ya Corona nchini, Serikali imeamua kulegeza masharti ya ugonjwa huu yaliyokuwa yamewekwa tangu mwaka 2020" Amesema Waziri huyo.

Mapema mwaka 2020 Zambia iliweka masharti ya kuzuia mikusanyiko katika nyumba za ibada, sehemu za starehe ili kuweza kupambana na kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Hadi sasa jumla ya visa 209,000 vimethibitishwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huku vifo vikiwa ni 3,650.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live