Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia yafikia makubaliano ya kurekebisha deni lake la mabilioni ya dola

Zambia Yafikia Makubaliano Muhimu Ya Kurekebisha Deni Lake La Mabilioni Ya Dola Zambia yafikia makubaliano muhimu ya kurekebisha deni lake la mabilioni ya dola

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Voa

Zambia Jumatatu ilitangaza kwamba imeingia makubaliano ya kihistoria na wakopeshaji binafsi wanaomiliki Eurobond zenye thamani ya dola bilioni 3.5, na kuondoa kikwazo kikubwa katika marekebisho ya muda mrefu ya deni la nchi hiyo.

“Historia imeandikwa. Tunayofuraha kutangaza makubaliano na wamiliki wa Eurobond”, Rais Hakainde Hichilema alisema kwenye mtandao wa X.

“Hii ni kurekebisha deni la zaidi ya dola bilioni 3.5 chini ya mfumo wa pamoja wa G20,” aliongeza.

Zambia, mzalishaji mkubwa wa shaba barani Afrika, ilishindwa kulipa deni lake la nje la dola bilioni 18.6 mwaka wa 2020 lakini mazungumzo yalikwama juu ya tofauti kati ya China na wakopeshaji wa nchi za Magharibi.

Hichilema alisema mwezi Disemba kwamba asilimia 98 ya wakopeshaji rasmi sasa wamesaini makubaliano ya awali ya kurekebisha deni la Zambia ambalo lilikadiriwa kufikia dola bilioni 32.8 mwaka 2022.

Chanzo: Voa