Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia yabaini ongezeko la deni trilioni 4.16

Zambia Pcddd Zambia yabaini ongezeko la deni trilioni 4.16

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali mpya ya Zambia, imebaini ongezeko la deni zaidi ya dola bilioni 2 sawa na trilioni 4.16 za kitanzania kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa tofauti na dola bilioni 6 zinazodaiwa na China sawa na trilioni 13.83 kama ilivoelezwa hapo awali.

Imesema kuwa taifa hilo linadaiwa jumla ya dola bilioni 14 sawa na trilioni 32.27 za kitanzania ambazo zimekopwa katika kipindi cha nusu mwaka 2021 kiasi ambacho kinazidi pato la taifa hilo kwa mwaka.

Hata hivyo fedha hizo zilikopwa kipindi cha utawala wa Rais Edgar lungu aliyetoka madarakani mwezi Augost 2021.

Nae Rais wa sasa Hakainde Hichilema yupo kwenye mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kufuatia taifa hilo kushindwa kulipa mikopo iliyotolewa kipindi cha Corona.

Lungu anatuhumiwa kukopa fedha nyingi ambazo alidai kuzielekeza katika kuboresha miundo mbinu katika kipindi cha utawala wake wa miaka 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live