Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia wazindua sera ya nyukilia

Aa58f86631c8117d3b60d60c99c0cfbf Zambia wazindua sera ya nyukilia

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ZAMBIA imezindua sera ya nyuklia itakayotoa mwongozo kwa mpango wa kitaifa wa nyuklia wa nchi hiyo.

Sera hiyo ya kitaifa ya nyuklia pia inalenga kulifanya taifa hilo la kusini mwa Afrika kuwa katika nafasi ya kutumia teknolojia ya nyuklia.

Hayo yalibainishwa juzi na Waziri wa Elimu ya Juu wa nchi hiyo, Brian Mushimba wakati wa uzinduzi wa sera hiyo.

Mushimba alisema sera hiyo itaiongoza Zambia katika kutekeleza programu za nyuklia ambazo zitalinda maisha ya watu na mazingira. Alisema uzinduzi huo ni ishara kwamba taifa hilo liko katika nafasi ya kuanza kutumia teknolojia ya nyuklia katika matumizi ya sayansi na teknolojia.

Alisema kuwa ushahidi unaonesha kwamba nchi ambazo zimejikita kwenye matumizi ya sayansi ya nyuklia zimekuwa na maendeleo ya kiteknolojia kwenye sekta mbalimbali. Alisema matumizi ya teknolojia ya nyuklia yatakuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya afya, kilimo, madini na nishati.

Mushimba alisema pamoja na mambo mengine, sera hiyo inatarajiwa kuimarisha mfumo wa kisheria, taasisi na utendaji wa sayansi na teknolojia ya nyuklia nchini humo.

Baraza la Mawaziri la Zambia liliidhinisha sera hiyo mwezi uliopita kutokana na kuwepo kwa hoja kwamba licha ya Serikali kutumia sayansi na teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo tangu mwaka 1969 lakini nchi hiyo haikuwa na sera inayosimamia matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Alisema Zambia imekuja na programu hiyo ya nyuklia ambayo itawezesha kujengwa kwa kituo cha sayansi na teknolojia ya nyuklia pamoja na kujenga mtambo wa nishati wa nyuklia.

Chanzo: habarileo.co.tz