Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakzaky: Mauaji ya halaiki ya Gaza yanaonesha udhaifu wa Israel

Umoja Wa Mataifa Unaomba Dola Milioni 294 Dharura Ya Wapalestina Zakzaky: Mauaji ya halaiki ya Gaza yanaonesha udhaifu wa Israel

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema mauaji makubwa ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza yameonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel una udhaifu mkubwa.

Sheikh Ibrahim Zakzaky amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Iran Press na kueleza kuwa: Mauaji ya raia huko Gaza yanaonesha udhaifu wa Wazayuni.

Kiongozi huyo mashuhuri wa kidini wa Nigeria hata hivyo amesisitiza kuwa, hakuna shaka mrengo wa muqawama wa Palestina utaibuka mshindi mkabala wa utawala haramu wa Israel.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amebainisha kuwa, "Tumedurusu mafunzonjia, mbinu za Imam Khomeini (MA) na kuzitekeleza katika nchi yetu." Hata watoto wadogo hawakusazwa na jinai za Israel Gaza

Sheikh Ibrahim Zakzaky amebainisha kuwa, iwapo maeneo mengine ya dunia yatataka kufahamu siri na njia za Imam Khomeini (MA), basi yuko tayari kuwabainishia njia hiyo.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa, jinai zinazoendelea kufanywa dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza kwa mara nyingine zimefichua udhaifu wa utawala wa Kizayuni.

Zaidi ya Wapalestina 3,500 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 13,000 kujeruhiwa kutokana na hujuma na mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza tokeo Oktoba 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live