Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu milioni 20 wauawa mapigano DRC

M23 Kuuteka Mji Muhimu Wa Uchimbaji Madini DRC Zaidi ya watu milioni 20 wauawa mapigano DRC

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya raia 20 wanaripotiwa kuuawa katika mashambulizi tofauti mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako mapigano yalianza tena mwishoni mwa juma kati ya vikosi vya serikali na waasi wa kkundi la M23.

Katika jimbo la Ituri, wanamgambo wa CODECO -kundi linalodai kulinda jamii ya Lendu kutoka kwa kabila lingine, Hema- lilishutumiwa kwa kulenga vijiji vitano vya Mahagi mapema siku ya Jumamosi.

Takriban watu tisa waliripotiwa kuuawa huko Nguli jirani ya Kivu Kaskazini na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), kundi ambalo linahusishwa na kundi la kigaidi la Daesh.

Katika taarifa yake, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilisema wapiganaji wa M23 walishambulia kwa akali vituo vyake sita na kulaani "ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji mapigano".

Kundi la Daesh limetangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusikana na mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live