Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu milioni 180 kukumbwa na janga la njaa Jangwa la Sahara

Aklfjqk Zaidi ya watu mil 180 kukumbwa na janga la njaa Jangwa la Sahara

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: Nipashe

ZAIDI ya watu milioni 180 waishio Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaweza kukumbwa na baa la njaa endapo shughuli za uzalishaji gesi joto utaendelea.

Hata hivyo ni asilimia nne tu ya uzalishaji gesi joto unazalishwa kwenye Nchi za Jangwa la Sahara huku asilimia 96 ikizalishwa kwenye nchi zilizoendelea.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Taasisi ya Green Faith International nchini Tanzania, Baraka Lenga amesema ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi yachangia uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kupungua hivyo kusababisha baa la nja.

Kutokana na hali hiyo, Lenga amesema Mkutano Mkuu wa 26 wa Umoja wa Mataifa unaojadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu sana kwa sababu unawaleta pamoja wafanyabiashara na wakuu wa nchi, wanaharakati na wanasiasa pamoja na taasisi zisizokuwa za kiserikali kujadili kwa pamoja ni kwa namna gani wanaweza kuepukana na mabadiliko hayo ambayo yanaweza kusababisha maafa kwa jamii.

Amesema kwa mujibu wa Mkataba wa makubaliano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi ni kuhakikisha jotoridi halipandi kuzidi kiwango cha digrii 1.5 na kwamba likienda mbali zaidi lisipande hadi digrii mbili.

Amedai endapo jotoridi likienda zaidi ya hapo kutaisababishia dunia kwenye matatizo makubwa kutokana ya kuingia kwenye wimbi la ukame na jangwa.

“Nchi 196 zilisaini mkataba huo na kupatiwa majukumu ya kwenda kuorodhesha na kupambana na uzalishaji wa gesi joto ambazo ndio zinaharibu mfumo wa hali ya hewa na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi katika mkataba huo ilionekana nchi nyingi zilizoendelea ndizo zinachangia kwa asilimia 96 ya mabadiliko ya tabia nchi huku nchi ambazo hazijaendelea zimechangia kwa asilimia nne,” amesema Lenga.

Amedai kuwa mkutano unaondelea ni wa muhimu sana kwani utatoa suluhisho la wapi tunaelekea sambamba na kupatiwa fedha kutoka nchi zilizoendelea ili kuhimili na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema mwaka 2018 katika Mkutano Mkuu wa 24 wa mabadiliko ya tabia nchi wanasayansi walitahadharisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yatasababisha watu zaidi ya milioni 122 kuingia kwenye umasikini katika kipindi kifupi kijacho.

Ameongeza kuwa uzalishaji wa chakula kusini mwa jangwa la Sahara utapungua kutoka asilimia 21 hadi asilimia tisa ifikapo mwaka 2080 kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo, Afisa Maji wa Bonde la Ziwa Rukwa, Grace Chatanda amesema miongoni mwa mikakati katika kuendeleza uhifadhi na vyanzo vya maji ni kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

Amesema shughuli za kibinadamu zinachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi hivyo aliwaomba wananchi kuacha kufanya shughuli za kilimo, uvuvi na uchomaji misitu.

Chanzo: Nipashe