Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya watu 50 wauawa shambulizi Burkina Faso

Mashambulizi 50 Burknafaso.jpeg Zaidi ya watu 50 wauawa shambulizi Burkana Faso

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa watu wasiopungua 50 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha katika kijiji kimoja kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lionel Bilgo, washambuliaji hao walishambulia usiku wa kuamkia Jumapili katika kijiji cha Seytenga ambacho kiko katika mkoa wa Seno ulioko maeneo ya mpakani ambako wanamgambo wenye mfungamano na magenge ya kigaidi ya Al Qaeda na DAESH (ISIS) wanahusika na mashambulio ya kutumia silaha.

Bilgo amefafanua kuwa hadi sasa jeshi limepata maiti za watu 50 baada ya kijiji cha Seytenga kushambuliwa Jumamosi usiku na kuongeza kuwa idadi ya vifo "inaweza kuongezeka".

Lakini mbali na takwimu zilizotolewa na msemaji wa serikali ya Burkina Faso, afisa mmoja wa usalama amevieleza vyombo vya habari hapo kuwa watu wasiopungua 100 wameuawa huku raia mmoja katika eneo la tukio ambaye hakutaka kutajwa jina lake akisema watu wapatao 165 wameuliwa katika hujuma hiyo.

Umoja wa Mataifa umelaani shambulio hilo ambalo umesema "limesababisha maafa ya roho za watu wengi" na kuzitolea mwito mamlaka husika za Burkina Faso kuwafikisha wahusika wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live